Kaunti ya Uasin Gishu ni mojawapo za kaunti za Kenya zilizobuniwa baada ya katiba mpya ya Jamhuri ya Kenya kupitishwa mwaka 2010. Uasin Gishu ni kaunti nambari 27 kulingana na orodha uliobuniwa kurahisisha utambulizi.
Wakati wa sensa uliofanyika mwaka 2019 ,idadi ya wakaazi ilikuwa 1,163,186 katika eneo la km2 3,392.2, msongamano ukiwa hivyo wa watu 343 kwa kilometa mraba[1].
Makao makuu yako Eldoret.