Kibisi | ||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
![]() | ||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||
| ||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||
Jenasi 6:
|
Vibisi ni ndege wa maji wa familia ya Podicipedidae. Domo lao jembamba kuliko mabata lina ncha kali. Vibisi huzamia majini ili kukamata samaki. Hujenga tago lao kwa matete linaloelea juu ya maji na hulifungia tete au mmea mwingine wa maji. Jike huyataga mayai 2-7. Kwa kawaida makinda wana milia na mara nyingi hubebwa mgongoni kwa mzazi.