Kifriuli (kwa lugha hiyo Furlan; kwa Kiitalia Friulano) ni mojawapo ya lugha za Kirumi, tawi la lugha za Kihindi-Kiulaya inayotumiwa na watu 600,000 hivi, ambao kati yao 300,000 ndiyo lugha mama yao, wakiwemo hasa Waitalia wa mkoa wa Friuli-Venezia Giulia, kaskazini mashariki mwa rasi ya Italia.