Our website is made possible by displaying online advertisements to our visitors.
Please consider supporting us by disabling your ad blocker.

Responsive image


Kiganja

Kiganja pamoja na vidole:
1 Kidole gumba, 2 Kidole cha shahada,
3 Kidole kirefu, 4 Kidole cha pete, 5 Kidole cha mwisho
Tupaia javanica, Homo sapiens

Kiganja (pia: kitengele) ni sehemu ya mwisho ya mkono inayoishia kwa vidole. Inaunganishwa kwa kifundo cha mkono na kigasha. Mguu una kiganja pia, lakini afadhali kiitwe uwayo au unyayo.

Binadamu huwa na viganja viwili, kila kimoja huwa kwa kawaida na vidole 5. Mtu hutumia kiganja na vidole vyake kwa kushika vitu na kutumia vifaa vingi. Kiganja cha mguu ni muhimu kabisa kwa kuweza kukaa wima na kutembea.

Sehemu ya ndani ya kiganja cha mkono ni kofi.

Mtu akikunja vidole pamoja na kiganja ngumi (sumbwi) inapatikana inayotumiwa kwa kupiga kwa ukali kwa mfano wakati wa mchezo wa ngumi.


Previous Page Next Page






Hand AF እጅ AM Man AN Hand ANG يد Arabic ܐܝܕܐ ARC Mano AST Otcitci ATJ Ampara AY Əl AZ

Responsive image

Responsive image