Kigweno (pia huitwa Kighonu) ni lugha ya Kibantu nchini Tanzania inayozungumzwa na Wagweno. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kigweno iko katika kundi la E60. Lugha ya Kigweno huingiliana na lugha ya Kikamba na lugha ya Kichaga kwa kiasi fulani.
Mwaka wa 2006 idadi ya wasemaji wa Kigweno imehesabiwa kuwa watu 2200. Lugha inazungumzwa katika Wilaya ya Mwanga hasa katika maeneo ya Kifula, Kikweni, Lambo, Mangio, Masumbeni, Mcheni, Msangeni, Mwaniko, Simbomu, Vuchamana maeneo ya Shighatini kwa kiwango kidogo. Kutokana na uenezaji huu kuna dalili ya kuwa wazungumzaji wa Kigweno ni wengi kuliko ilivyoelezwa katika marejeo ya kitaalamu yaliyotajwa hapo juu. Tarafa yote ya Ugweno huzungumza Kigweno kama Lugha mama na Kiswahili ni lugha ya pili.
Wagweno wakati mwingine huweza kuwa mahiri wa kuzungumza lugha ya Kipare ambapo Wapare wao hawajui Kigweno wao hubakia na lugha moja tu ya Kipare ambacho huzungumzwa Usangi na maeneo ya Mwanga yaani tambarare na maeneo ya Wilaya ya Same.
Wagweno wana ngoma zao zinazoitwa mdumange ambazo huchezwa usiku kwa kutumia mianzi (mirangikwa kwa Kigweno) kama ile inayoitwa "nakuokera karughu vamaie kasembelele..." Sifa kuu ya Wagweno lugha yao haitumiki sana kwenye matambiko maana watambikaji wote hutumia lugha ya Kipare wanapokuwa katika mambo yao ya mila.