Kijita (pia huitwa Echijita) ni lugha ya Kibantu nchini Tanzania inayozungumzwa na Wajita. Mwaka wa 2005 idadi ya wasemaji wa Kijita ilihesabiwa kuwa watu 205,000. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kijita kiko katika kundi la E20.