Kikerewe (au Kikerebe) ni lugha ya Kibantu nchini Tanzania inayozungumzwa na Wakerewe. Mwaka wa 1987 idadi ya wasemaji wa Kikerewe imehesabiwa kuwa watu 100,000. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kikerewe iko katika kundi la E20.