Kikuria (kwa lugha yenyewe: Igikuria) ni mojawapo ya lugha za Kibantu inayoongelewa na kabila la Wakurya nchini Tanzania na Kenya[1].
Mwaka wa 2005 idadi ya wasemaji wa Kikuria nchini Tanzania imehesabiwa kuwa watu 430,000. Pia kuna wasemaji 260,000 nchini Kenya.
Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kikuria iko katika kundi la E40.
Maho (2009) anahesabu Kisimbiti, Kihacha, Kisurwa na Kisweta kama lugha tofauti, si lahaja za Kikurya tu.
Alfabeti ya Kikuria [2] | |||||||||||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
A | B | Ch | E | Ë | G | H | I | K | M | N | Nd | Ny | Ng' | O | Ö | R | Rr | S | T | U | W | Y | |||||
a | b | ch | e | ë | g | h | i | k | m | n | nd | ny | ng' | o | ö | r | rr | s | t | u | w | y |