Kiluguru ni lugha ya Kibantu inayozungumzwa na Waluguru nchini Tanzania. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kiluguru kiko katika kundi la G30.
Mwaka wa 2001 idadi ya wasemaji wa Kiluguru imehesabiwa kuwa watu 692,000. Lugha hii huzungumzwa hasa na Waluguru wanaopatikana katika mkoa wa Morogoro ambao ni wazawa. Sehemu maarufu kwa kuzungumzwa lugha hii ni: Matombo (inayojumuisha Tawa, Kibogwa, Milawilila, Uponda, Kitungwa, Konde, Kiswira), maeneo mengine ni tarafa ya Mgeta.
Mfano wa lugha: Hausindile maana yake Umeshindaje, Ukae maana yake Nyumbani, Imwana kolila maana yake mtoto analia.