Kwa matumizi mengine ya jina hili tazama Kilwa
Kata ya Kilwa Masoko | |
Nchi | Tanzania |
---|---|
Mkoa | Lindi |
Wilaya | Kilwa |
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 21,519 |
Kilwa Masoko ni mji mdogo katika Tanzania ulio makao makuu ya Wilaya ya Kilwa tangu miaka ya 1960.
Iko barani ikitazama Kilwa Kisiwani. Mji ni wa kisasa. Kuna uwanja mdogo wa ndege pia bandari ndogo yenye kituo cha forodha.
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 21,519 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 13,601. [2] walioishi humo.
Msimbo wa posta ni 65408.