Kimadi (au Kigira) ni lugha ya Kivuka-Guinea Mpya nchini Papua Guinea Mpya inayozungumzwa na Wamadi. Mwaka wa 2003 idadi ya wasemaji wa Kimadi imehesabiwa kuwa watu 380, na lugha imekaribia kutoweka kabisa hivi karibuni. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kimadi iko katika kundi la Kifinisterre.