Kimalay ni lugha ya Kiaustronesia nchini Malaysia, Brunei, Singapuri na Indonesia inayozungumzwa na Wamalay. Ni lugha ya mawasiliano kwa wengi, hata nchini Ufilipino, Timor Mashariki na Uthai, tofauti na Kimalay Sanifu ambayo ni lugha rasmi nchini Malaysia.
Mwaka wa 2007 idadi ya wasemaji wa Kimalay kama lugha mama ilihesabiwa kuwa watu milioni 77, lakini wasemaji wote wanaweza kufikia milioni 200-290.
Kufuatana na uainishaji wa lugha wa ndani zaidi, Kimalay iko katika kundi la Kimalayiki.