Kimalay ya Bali ni lugha ya Kiaustronesia nchini Indonesia inayozungumzwa na Wamalay kwenye kisiwa cha Bali. Mwaka wa 2000 idadi ya wasemaji wa Kimalay ya Bali imehesabiwa kuwa watu 25,000. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kimalay ya Bali iko katika kundi la Kimalayiki. Wengine huiangalia kama krioli.