Kimbugwe ni lugha ya Kibantu nchini Tanzania inayozungumzwa na Wambugwe. Mwaka wa 1999 idadi ya wasemaji wa Kimbugwe imehesabiwa kuwa watu 24,000. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kimbugwe iko katika kundi la F30. Lugha ya Kimbugwe inafanana na Kirangi, na Warangi wengi wanadai kwamba Kimbugwe ni lahaja ya Kirangi tu. Kisayansi lakini Kimbugwe ni lugha yenyewe kwa vile asilimia 74 tu za msamiati wake zina chanzo kimoja na Kirangi. Wasemaji wakikutana wanagundua kuwa lugha hizo mbili hazitambulikani moja kwa nyingine bila kujifunza ile nyingine.