Kimeru (au Kirwa) ni lugha ya Kibantu nchini Tanzania inayozungumzwa na Warwa. Isichanganywe na lugha ya Kimeru nchini Kenya. Mwaka wa 1987 idadi ya wasemaji wa Kimeru imehesabiwa kuwa watu 90,000. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kimeru iko katika kundi la E60.