Kindali (au Chindali) ni lugha ya Kibantu nchini Tanzania inayozungumzwa na Wandali. Mwaka wa 1987 idadi ya wasemaji wa Kindali nchini Tanzania imehesabiwa kuwa watu 150,000. Pia kuna wasemaji 70,000 nchini Malawi (2003). Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kindali iko katika kundi la M20.