Kindonde (au Kimawanda) ni lugha ya Kibantu nchini Tanzania inayozungumzwa na Wandonde. Mwaka wa 2002 idadi ya wasemaji wa Kindonde imehesabiwa kuwa watu 10,000. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kindonde iko katika kundi la P20. Imefikiriwa kufanana na Kimwera.