Kinyambo (au Orunyambo) ni lugha ya Kibantu nchini Tanzania inayozungumzwa na Wanyambo. Mwaka wa 2003 idadi ya wasemaji wa Kinyambo imehesabiwa kuwa watu 400,000. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kinyambo iko katika kundi la E20.