Kinyamwezi ni lugha ya Kibantu nchini Tanzania inayozungumzwa na Wanyamwezi. Mwaka wa 2006 idadi ya wasemaji wa Kinyamwezi imehesabiwa kuwa watu 980,000. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kinyamwezi iko katika kundi la F20. Inafanana na Kisukuma.