Kirufiji (au Kiruihi) ni lugha ya Kibantu nchini Tanzania inayozungumzwa na Warufiji. Mwaka wa 1987 idadi ya wasemaji wa Kirufiji imehesabiwa kuwa watu 200,000. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kirufiji iko katika kundi la P10.