Kirumanj (kwa lugha yenyewe Rumantsch, Romansch au Romanche) ni moja kati ya lugha za Kirumi na kati ya lugha nne za kitaifa nchini Uswisi pamoja na Kijerumani, Kifaransa na Kiitalia.
Kirumanj hufanana na Kiitalia.
Idadi ya wasemaji ni takriban watu 50,000 katika jimbo la Graubünden. Wasemaji wako hasa vijijini katika milima ya Alps.