Kisiwa cha Man (kwa Kimanx: Ellan Vannin; kwa Kiingereza: Isle of Man) ni kisiwa kilichopo baharini kati ya Uingereza na Eire chenye wakazi 75,000 kwenye eneo la km² 572.
Man ni eneo chini ya taji la Uingereza, si sehemu ya Ufalme wa Muungano wenyewe.
Lugha rasmi ni Kiingereza pamoja na Kimanx ambacho ni lugha ya Kikelti. Hakuna tena wasemaji wa Kimanx kama lugha ya kwanza, lakini inafundishwa shuleni.