Kisukuma ni lugha ya Kibantu nchini Tanzania inayozungumzwa na Wasukuma. Mwaka wa 2006 idadi ya wasemaji wa Kisukuma imehesabiwa kuwa watu 5,430,000. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kisukuma iko katika kundi la F20. Inafanana na lugha ya Kinyamwezi.