Kitamili ni lugha ya Uhindi inayojadiliwa hasa kwenye jimbo la Tamil Nadu pamoja na kaskazini ya Sri Lanka. Ni kati ya lugha kubwa za dunia yenye wasemaji zaidi ya milioni 70.
Kitamili huhesabiwa kati ya lugha za Kidravidi ambazo ni lugha asilia za Uhindi.
Kitamili imeandikwa tangu zaidi ya miaka 2000. Mfano ya kale ni ni mwandiko kwenye miamba ya mwaka 254 KK. Ni lugha ya pekee yenye umri mkubwa kama huu inayoendelea kutumiwa mfululizo hadi leo.