Kitemi (pia huitwa Kisonjo) ni lugha ya Kibantu nchini Tanzania inayozungumzwa na Watemi. Mwaka wa 2002 idadi ya wasemaji wa Kitemi imehesabiwa kuwa watu 30,000. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kitemi iko katika kundi la E40.