Kiungulia (kwa Kiingereza heartburn) ni hali ya kusikia maumivu makali katika koo la chakula.
Maumivu hayo yanatokana na kupanda kwa asidi iliyomo tumboni (asidi haidrokloriki = HCl) inayofanya kazi ya kuua vijidudu vinavyoingia tumboni kwa njia ya chakula na maji.
Mara nyingi kiungulia kikatokea baada ya tumbo kujaa gesi.
Kiungulia kinaweza kuwa na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kula kwa pupa au kupita kiasi, matumizi ya dawa za kulevya, ujauzito, tumbo kujaa gesi, vidonda vya tumbo n.k.