Kividunda ni lugha ya Kibantu nchini Tanzania inayozungumzwa na kabila dogo la Wavidunda, wanaoishi katika wilaya ya Kilosa, mkoa wa Morogoro. Mwaka wa 1987 idadi ya wasemaji wa Kividunda imehesabiwa kuwa watu 32,000. Kufuatana na uainishaji wa lugha za Kibantu wa Malcolm Guthrie Kividunda iko katika kundi la G30. Kinafanana hasa na Kiluguru, lakini pia na Kihehe na lugha nyingine za kandokando.