Krete (kwa Kigiriki Κρήτη, Kríti, matamshi ya kale, Krḗtē) ni kisiwa kikuu na chenye watu wengi zaidi cha Ugiriki, na ni cha tano katika Bahari ya Kati, baada ya Sicily, Sardinia, Cyprus na Corsica.
Pamoja na visiwa vya jirani vya bahari ya Aegean kinaunda mkoa wa Krete (Περιφέρεια Κρήτης), mmoja kati ya 13 ya nchi nzima. Mwaka 2011, mkoa huo ulikuwa na wakazi 623,065.
Mji mkuu na mji mkubwa ni Heraklion.
Krete ni sehemu muhimu ya ustaarabu na uchumi wa Ugiriki ukidumisha upekee wake katika utamaduni (kwa mfano upande wa ushairi na muziki).