Our website is made possible by displaying online advertisements to our visitors.
Please consider supporting us by disabling your ad blocker.

Responsive image


Krismasi

Picha takatifu ya Kiorthodoksi inayoonyesha kuzaliwa kwake Kristo. Yesu anaonekana amevikwa sanda na kulazwa kaburini, kwa maana alizaliwa ili awakomboe watu kwa kifo chake.

Krismasi (pia Noeli) ni sikukuu ambayo Wakristo wengi husheherekea kuzaliwa kwake Yesu Kristo zaidi ya miaka 2000 iliyopita.

Kwa kawaida husheherekewa tarehe 25 Desemba katika Ukristo wa magharibi[1] na tarehe 6 Januari katika ule wa mashariki.

Martyrologium Romanum inatangaza sherehe hiyo kwa maneno haya ya fahari: "Karne nyingi baada ya uumbaji wa ulimwengu, ambapo mwanzo Mungu aliumba mbingu na dunia akaunda mtu kwa sura yake mwenyewe; tena karne nyingi tangu Aliye Juu, baada ya gharika kuu, alipong'arisha upinde wa mvua mawinguni kama ishara ya agano na amani; karne 21 baada ya Abrahamu, baba yetu katika imani, kuhama nchi ya Ur wa Wakaldayo; karne 13 baada ya taifa la Israeli kutoka Misri chini ya Musa; miaka elfu hivi baada ya Daudi kupakwa mafuta awe mfalme; katika juma la 65 kadiri ya utabiri wa Danieli; wakati wa Olimpiki ya 194; katika mwaka 752 tangu Roma uundwe; katika mwaka wa 42 wa utawala wa Kaisari Oktaviano Augusto, huku amani ikitawala duniani kote, Yesu Kristo, Mungu wa milele na Mwana wa Baba wa milele, akitaka kutakasa ulimwengu kwa ujio wake mtakatifu sana, kisha kutungwa mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu na kupita miezi 9, alizaliwa na Bikira Maria huko Bethlehemu wa Yuda akawa binadamu: ndiyo Noeli, Kuzaliwa kwa Bwana wetu Yesu Kristo katika mwili"[2].

  1. Martyrologium Romanum
  2. https://www.santiebeati.it/dettaglio/20650

Previous Page Next Page






Қьырса ныҳәа AB Хъуромэ ADY Kersfees AF Weihnachten ALS ገና AM Korismas AMI Nadal AN Crīstesmæsse ANG عيد الميلاد Arabic ܥܐܕܐ ܕܒܝܬ ܝܠܕܐ ARC

Responsive image

Responsive image