Kuchanyika | ||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||
| ||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||
Jenasi 7:
|
Kuchanyika ni ndege wadogo wa familia Cettiidae. Ndege hawa wanafanana na shoro, kucha na kuchamsitu, na zamani wote waliainishwa pamoja katika familia Sylviidae. Spishi nyingine za kuchanyika zina mkia mrefu, nyingine zina mkia mfupi sana. Zina rangi ya kahawia au kijivu mgongoni na nyeupe au njano chini; spishi kadhaa zina rangi kali (Tesia k.m.). Spishi za Cettia tu zinatokea Ulaya, nyingine zinatokea misitu ya Afrika na Asia. Hula wadudu. Hulijenga tago lao kwa umbo wa kikombe au kikapu kwa kigoga, nyuzinyuzi, mizizi na/au majani. Jike huyataga mayai 2-6.