Kukuziwa | ||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||
| ||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||
Jenasi 4 za kukuziwa: |
Kukuziwa ni ndege wa jenasi mbalimbali katika familia Rallidae. Wana mnasaba na viluwiri lakini ni ndege wa maji wa kweli (tazama shaunge pia). Wanaachana na viluwiri kwa kuwa na kigao kidogo juu ya domo. Rangi yao ni nyeusi au kijivu nzitu na mabawa ya spishi nyingi yana rangi ya kahawa. Rangi ya domo na kigao ni nyeupe au nyekundu. Vidole vyao vina ndewe, siyo ngozi kama mabata, ili kusogeza mbele kwa urahisi majini. Hula mimea, wanyama wadogo na mayai. Hujenga tago kubwa kwa mimea majini au ardhini na huyataga mayai 6-12.