Kumbukumbu ni hali ya kuweza kutambua jambo uliloliona au kuweza kufafanua au kuelezea jambo ulilolihifadhi ndani ya kichwa chako. Mtu, na hata mnyama, huweza kukumbuka kitu, jambo, hali, sehemu, wakati n.k. Mfano: mwanafunzi husoma vitabu lakini baadaye itambidi kujibu na kuelezea kile alichokisoma.
Binadamu wanatofautiana katika uwezo wa kufikiri kwa sababu ya mambo mbalimbali. Mambo hayo ni pamoja na akili yenyewe, msongo wa mawazo, akili ya kusahau, kuijaza mambo mengi, kazi afanyayo mtu, umbile kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
Yapo madhara yanayoweza kusababisha mtu kuwa na uwezo mdogo wa kufikiri na kukumbuka yale aliyoyahifadhi katika akili yake; mambo hayo ni: mlo mbovu wa chakula, hasa vyakula vile vyenye mafuta mengi: mfano, chips, baga n.k.
Pia akili ya binadamu hutambuliwa kutokana na matendo anayofanya katika maisha yake ya kila siku.
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kumbukumbu kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |