Kumi ni namba inayoandikwa 10 kwa tarakimu za kawaida lakini X kwa zile za Kirumi na ١٠ kwa zile za Kiarabu. Inafuata 9 na kutangulia 11.
Vigawo vyake vya namba tasa ni: 2 x 5.
Namba kumi ni msingi wa mahesabu mengi, kutokana na idadi ya vidole vya mikono ya binadamu.