Longyearbyen ni makao makuu ya utawala wa Norwei kwenye visiwa vya Svalbard. Mji huu mdogo uko kwenye kisiwa cha Spitsbergen.
Longyearbyen ni kati ya makazi ya kibinadamu ya kaskazini kabisa duniani. Kwa jumla kuna wakazi 1,800 wengi wao Wanorwei na wengine Warusi.
Mji ulianzishwa mnamo 1906 kama makazi ya wafanyakazi wa migodi ya makaa mawe.