Maabadi ni mahali popote pa kufanyia ibada, kama vile hekalu, kanisa, msikiti, patakatifu n.k.
Pia tunaweza kusema ni sehemu iliyowekwa wakfu au ni eneo maalum lililojengwa ambalo mtu au kundi la watu kama vile kusanyiko hukutana kufanya ibada au kujifunza masomo ya kidini. Jengo lililojengwa kwa lengo hili wakati mwingine huitwa nyumba ya ibada.
Chini ya Sheria ya Kimataifa ya Kibinadamu[1] na Mikataba ya Geneva[2] nyumba za ibada hupewa ulinzi maalum sawasawa na ulinzi unaotolewa kwa hospitali kwa kuonyesha msalaba mwekundu.