Maarifa (kutoka neno la Kiarabu; kwa Kiingereza: competence) ni njia inayotumiwa kujitoa katika shida ama kuweza kupata kitu, kwa kutumia elimu au ujuzi. Ujuzi huo unaweza ukawa wa kuzaliwa nao au ukatokana na mang'amuzi ya maisha yakiwa pamoja na kusoma, kusikia au kutenda.
Pia huhusisha ufahamu na uelewa, hususani wa ukweli, kama ulivyofundishwa au kuthibitishwa na Roho Mtakatifu.
Neno hilo linatumika pia kudokeza mbinu za ushirikina katika kufanikisha mambo kadiri ya matakwa ya mtu.
Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |