Majira (kutoka neno la Kiarabu) au msimu ni sehemu ya mwaka ambayo ina tabia za pekee upande wa hali ya hewa.
Katika Dunia, majira yanapatikana kutokana na sayari hiyo kuligunzuka Jua na kuwa na mhimili usio wima.
Katika Afrika Mashariki mara nyingi yanajitokeza zaidi majira mawili ambayo ni majira ya mvua na kiangazi.
Katika maeneo yaliyo mbali na ikweta yanahesabika majira manne: majira ya kuchipua, majira ya joto, majira ya kupuputika majani na majira ya baridi.