Malaika mkuu (kwa Kigiriki ἀρχάγγελος arkh+angelos)[1] ni jina la heshima kwa baadhi ya malaika wenye hadhi ya juu kati ya viumbe vya kiroho.
Msingi wa imani hiyo ni kwamba kila malaika ameumbwa peke yake na tofauti na wengine wote, na kwamba katika kumtumikia Mungu aliyewaumba wanashirikiana kwa ngazi.