Matope ni mchanganyiko wa maji na udongo ambao unatengeneza ujiuji mzito.
Mara nyingi matope hutokea endapo mvua imenyesha sehemu yenye vumbi au udongo au maji mengi kumwagwa sehemu yenye vumbi kama wakati wa utengenezaji wa barabara.
Ni lazima barabara ichimbwe au kuchongwa kabla ya kuanza kutengenezwa; wakati huo ndipo matope hutokea.
Pia matope hupatikana sana sehemu za mabwawa, madimbwi, maziwa na sehemu nyingine ambazo hukusanya maji mengi kutoka kwenye vyanzo mbalimbali kama vile mito, chemchemi na mvua.
Udongo wa mfinyanzi ukichanganywa na maji unafaa kutengenezea vitu mbalimbali, hata kujenga nyumba za udongo au za matofali.
Matope, hasa ya moto, yanatumika pia kama tiba ya baridi-yabisi.