Mgahawa (au mkahawa kutoka kinywaji "kahawa") ni mahali ambapo chakula kilichopikwa kinauzwa kwa umma, na ambapo watu huketi katika viti maalum vilivyoandaliwa pamoja na meza na kula.
Migahawa hiyo huwa na vyakula tofauti, kwa mfano wali, nyama,biliani, viazi, mayai n.k.
Pia migahawa huwa na vinywaji kama vile kahawa, soda, maji, maziwa,juisi, chai n.k.
Migahawa hiyo hupatikana kwa wingi mjini kwa mfano katika shule,ofisi n.k.
Mgahawa hutoa huduma yake kwa bei ya kawaida. Baadhi ya watu ambao hupendelea kula kwenye migahawa ni wanafunzi, walimu n.k.
Mgahawa ni sehemu ambayo watu huweza kupata chakula au vinywaji kwa haraka na urahisi, bila kutumika/kutumia nguvu zao wenyewe.
Kwa kawaida ilivyozoeleka huwa kuna mtu wa kuhudumia mahitaji ya wateja kwa makubaliano ya mhudumiwa kulipia huduma anayohitaji.
Kwa kweli hakuna rekodi sahihi za mwaka au nyakati gani za kuonyesha hasa ni lini mwanzo wa utamaduni au namna hii ya kubadilishana huduma.
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mgahawa kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |