Our website is made possible by displaying online advertisements to our visitors.
Please consider supporting us by disabling your ad blocker.

Responsive image


Michezo

Mashindano ya mbio ya masafa marefu sana, maarufu kama Marathon.

Michezo ni amali au mazoezi ya kimwili ambayo mara nyingi yana ushindani ndani yake. Yanatendeka kufuatana na kawaida na taratibu maalumu zilizokubaliwa kati ya wachezaji au katika jamii.

Michezo ni ya aina nyingi ikiwemo michezo ya juu angani, majini, kwenye nchi kavu na pia kwenye barafu. Watu hushiriki kwenye michezo kushindania zawadi, kama aina ya mazoezi au kujiburudisha tu.

Mifano maarufu ya michezo ni mpira wa miguu, mpira wa kikapu, mpira wa mkono, mpira wa magongo, aina za mbio, mashindano ya kuogelea na kadhalika.

Watu wengi hupenda kutazama mashindano ya michezo. Tabia hii imekuwa msingi kwa wachezaji wanaotekeleza michezo yao si kwa kujiburudisha, bali kikazi na kwa malipo, pengine makubwa ajabu.

Tangu kale watu wamekutana kwa mashindano makubwa ya michezo kati ya jamii, makabila au mataifa. Kati ya mashindano mashuhuri hasa ni Michezo ya Olimpiki iliyofanyika awali Ugiriki ya Kale na sasa inafanyika kwa ushiriki wa mataifa yote duniani kila baada ya miaka minne.

Kwa nchi ya Kenya michezo inayopendwa sana ni: kriketi, mbio za magari, mpira wa miguu, raga na ngumi.

Kwa nchi ya Tanzania michezo inayopendwa sana ni: mpira wa miguu, riadha, mpira wa pete, mpira wa wavu; pia kuna hamasa kubwa kwa watu kusoma magazeti kuhusu michezo ili kupata dondoo na habari muhimu kuhusu michezo mbalimbali inayoendelea huko viwanjani.


Previous Page Next Page






Аспорт AB Sport AF Sport ALS ስፖርት AM Esporte AN Plega ANG खेल ANP رياضة Arabic رياضة ARY رياضه ARZ

Responsive image

Responsive image