Milima ya Taita (kwa Kiingereza: Taita Hills, pia Teita Hills) iko kusini mashariki mwa Kenya, katika kaunti ya Taita-Taveta.
Ni sehemu ya milima ya Tao la Mashariki ambayo ina miaka zaidi ya milioni 100[1] .
Milima ni hasa mitatu: Dabida, Sagalla na Kasigau. Mkubwa zaidi ni Dawida ambao unafikia metre 2 228 (ft 7 310) juu ya usawa wa bahari katika kilele cha Vuria. Vingine ni: Iyale, Wesu, and Susu.