06°28′S 37°00′E / 6.467°S 37.000°E
Milima ya Ukaguru iko mashariki mwa Tanzania katika wilaya za Kilosa na Gairo mkoani Morogoro ambapo milima ya Rubeho ipo wilaya ya Gairo na milima ya Ukaguru ipo wilaya ya Kilosa; mto Mkondoa ndio unaotenganisha milima hiyo.
Kilele cha juu kiko mita 806 juu ya usawa wa bahari.
Jina linatokana na kabila la Wakaguru ambao ndio wenyeji wa eneo hilo. Ndipo mahali ambapo walitia nanga baada ya safari yao ndefu kutoka nchini Rwanda.
Ni sehemu ya milima ya Tao la Mashariki.