6°6′22″S 38°40′36″E / 6.10611°S 38.67667°E
Mkange ni kata ya Wilaya ya Chalinze katika Mkoa wa Pwani, Tanzania, yenye postikodi namba 61322. Mji wa kihistoria wa Saadani umo ndani ya eneo la kata hiyo.
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 15,151 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 12,026 [2] walioishi humo.
Reli ya Dar es Salaam kuelekea Arusha na Tanga inapita humo. Kuna mipango ya kutengeneza barabara kuu kati ya Mombasa na Dar es Salaam kufuatia mwambao wa Bahari ya Hindi[3] itakayopita kwenye kata hiyo.