Mkoa wa Tabora |
|
Mahali pa Mkoa wa Tabora katika Tanzania | |
Majiranukta: 5°30′S 32°50′E / 5.500°S 32.833°E | |
Nchi | Tanzania |
---|---|
Wilaya | 8 |
Mji mkuu | Tabora |
Serikali | |
- Mkuu wa Mkoa | ACP Advera John Bulimba |
Eneo | |
- Jumla | 76,151 km² |
Idadi ya wakazi (2022) | |
- Wakazi kwa ujumla | 3,391,679 |
Tovuti: http://www.tabora.go.tz/ |
Mkoa wa Tabora ni kati ya mikoa 31 ya Tanzania wenye postikodi namba 45000.
Makao makuu yako Tabora Mjini. Tabora ni jina la mji, wilaya na mkoa wa Tanzania ya kati.
Eneo la mkoa ni km2 76,151; mnamo km2 34,698 (46%) ni hifadhi ya misitu, km2 17,122 (22%) ni hifadhi ya wanyama.
Jumla ya wakazi ilikuwa watu 3,391,679 (2022[1]). Wenyeji wa Tabora ni hasa Wanyamwezi. Walio wengi ni wakulima na wafugaji.
Kuna wilaya 8 (katika mabano idadi ya wakazi mwaka 2022[2]): Tabora Mjini (308,741), Nzega Vijijini (574,498), Nzega Mjini (125,193), Igunga (546,204), Uyui (562,588), Urambo (260,322), Sikonge (335,686), Kaliua (678,447).
Jina la Urambo humkumbuka Mtemi Mirambo aliyekuwa mtawala muhimu wa Wanyamwezi kabla ya kuingia kwa ukoloni.