Mitume wa Yesu |
---|
|
Bartolomayo (kwa Kigiriki Βαρθολομαιος) alikuwa Myahudi wa karne ya 1, mmojawapo kati ya Mitume wa Yesu kadiri ya Injili Ndugu.
Wengi wanaona hilo ni ubini wake (kwa Kiaramu lina maana ya "mwana wa Tolomayo"), kumbe jina lake mwenyewe ni "Natanaeli", kama anavyotajwa na Injili ya Yohane 1:45, rafiki wa Mtume Filipo. Kama ni hivi, alikuwa mwenyeji wa Kana ya Galilaya, na unyofu wake ulisifiwa na Yesu mara alipokutana naye kwenye mto Yordani.
Anaheshimiwa na madhehebu karibu yote ya Ukristo kama mtakatifu, hasa tarehe 24 Agosti[1].