Muhammad (kwa Kiarabu "Mwenye kusifika sana"; jina kamili kwa kirefu ni
محمد بن عبد الله بن عبد ﺍﻟﻤﻄﻠﺐ ﺍﻟﻬﺎﺷﻤﻲ Muhammad bin 'Abd Allāh bin 'Abd al-Muţţalib al-Hāshimī; 570 hivi - 8 Juni 632) anaaminika katika dini ya Uislamu kuwa ni mtume wa mwisho wa Mungu (Allah) kwa binadamu.