Musoma | |
Mahali pa mji wa Musoma katika Tanzania |
|
Majiranukta: 1°29′24″S 33°48′0″E / 1.49000°S 33.80000°E | |
Nchi | Tanzania |
---|---|
Mkoa | Mara |
Wilaya | Musoma Mjini |
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 164,172 |
Msimbo wa posta | 31101 - 31113 |
Musoma ni mji wa Tanzania uliopo kwenye mwambao wa mashariki wa Ziwa Viktoria. Musoma imepata halmashauri na hadhi ya manisipaa. Manispaa hiyo inapakana na Wilaya ya Musoma Vijijini.
Ni makao makuu ya Mkoa wa Mara.
Katika sensa ya mwaka 2002, idadi ya wakazi wa mji huo ilihesabiwa kuwa 108,242 [1] na katika ile ya mwaka 2022 walihesabiwa 164,172 [2].