Mwambatope (kwa Kiingereza: shale rock) ni aina ya mwamba mashapo yenye chembe ndogo sana; asili yake ni mashapo ya matope.
Matope yanayofanya mwambatope ni ya udongo wa mfinyanzi (clay) pamoja na chembe ndogo za kwatzi na kalsiti.[1]
Mara nyingi mwambatope yanatokea kwa matabaka membamba yanayoweza kutenganishwa kirahisi. Kama aina hii ya mwambatope inaathiriwa na shinikizo na joto kubwa zaidi itakuwa mwamba metamofia aina ya grife unaovunjika kwa urahisi kwa bapa nyembamba kama sahani yaani sleti. Hizo zinatumiwa kama bapa za kuezeka mapaa ya nyumba.