Our website is made possible by displaying online advertisements to our visitors.
Please consider supporting us by disabling your ad blocker.

Responsive image


Nadharia ya uhusianifu

Nadharia ya uhusianifu iliundwa na Albert Einstein na inajumlisha nadharia ya uhusianifu maalumu (mwaka 1905) na nadharia ya uhusianifu ya jumla (1916).

Uhusianifu maalumu husema:

  • Wachunguzi wakiwa na mwendo tofauti, wakati na umbali hubadilishwa, katika fomula γ=(1-v2/c2)-1/2.
  • Kasi ya nuru huwa sawa kwa wachunguzi wote wenye kasi isiyobadilika.

Uhusianifu wa jumla huelezea mvutano kama mviringo wa nafasiwakati. Huendeleza nadharia ya uvutano ya Isaac Newton. Hutumiwa na fizikia ya ulimwengu ya kisasa.

Majaribio mengi yamethibitisha nadharia zote mbili,[1] kama vile majaribio ya Michelson-Morley na majaribio ya Ives-Stilwell (uhusianifu maalumu), na majaribio wa Pound-Rebka (uhusianifu wa jumla).

  1. http://www.edu-observatory.org/physics-faq/Relativity/SR/experiments.html

Previous Page Next Page